BENNO KAKOLANYA SIMAMA WEWE MWENYEWE.

Image may contain: 1 person, standing and outdoor
Mambo yaliharibika zaidi mara baada ya kuondoka George Lwandamina, timu ikawa chini ya Noel Mwandila akisaidiwa na Shadrack Nsajigwa 'Fusso' . . wachezaji kugoma ikawa kawaida, hadi anawasili Mwinyi Zahera hiyo tabia iliendelea! Yanga SC ikawa ina unga unga kikosi, si unakumbuka ile safari ya Algeria kucheza na USM Alger? timu ilipowasili JKNIA kocha wetu alishangazwa sana na jinsi timu inavoenda kienyeji licha ya kuwa Yanga ni timu kubwa.
Baada ya michuano ya SportPesa kule Kenya kumalizika ndipo kwa mara ya kwanza Mwinyi Zahera aliwaita wachezaji wake , namnukuu
"Hii ni kazi na mnapaswa kuiheshimu, mnafahamu fika timu haina hela nataka tukubaliane kama huwezi kucheza bila kulipwa pesa yako basi naomba mapema kabisa nikuruhusu uondoke, ninyi mliomaliza mikataba yenu na bado mnatamani kuendelea hapa ningewashauri nyie sinyeni Yanga hela yenu mtaipata tu japo yawezekana isiwe leo ama kesho "
Baada ya hapo Mwalimu akawapa muda wachezaji wa kufikiri na kwenda kushauriana na watu wao wa karibu, Wachezaji wote waliridhia kuwa wapo tayari kuipigania Yanga licha ya changamoto za kipesa ndipo wengine wakasaini hata bila signing fees! Hapo ndipo Yanga ikawa kitu kimoja pasipo kuangalia sana maslahi ya kifedha, ukiwa na shida ya kipesa unamweleza mwalimu naye anatoa pesa yake na kukupatia, furaha ikarudi na umoja ukajengeka siku hadi siku.
Usiku wa kuamkia tarehe 4 November, 2018 majira ya saa 7 usiku timu ikiwa hotelini kocha mkuu akagongewa mlango na meneja wa timu! hata kabla ya kufungua kocha akasikia " Kocha, Kocha Benno anaondoka" . . . Zahera akafungua mlango haraka kisha akawaambia naomba mwiteni Benno, muwahini haraka! ndipo Benno akarudi na kukaa chumbani kwa kocha kwa maongezi.
"Benno kulikoni unataka kuondoka? tumefanya kikao saa 5 usiku kama una tatizo si ungenambia muda ule iweje usubiri tukiwa tumelala ndipo utoroke? kumbuka kama timu tulikubaliana kuwa tupo tayari kufanya kazi licha ya ukata, iweje utusaliti na unajua fika kesho tuna mechi ngumu dhidi ya Ndanda. . nakuomba baki hapa kama una shida sana tutaongea naomba tufocus kwa mchezo wa ujao kwanza" , Benno aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa anaondoka, kuangalia nje kumbe tayari meneja wake amekuja kumchukua.
Simu za viongozi wala kocha akawa hapokei, baada ya wiki meneja wake akajitokeza kuwa anaupa uongozi wa Yanga siku 3 uwe umemlipa mteja wake la sivyo Benno atakuwa mchezaji huru! Siku tatu zikapita kisha wiki ikakatika ndipo Benno kwa kushirikiana na meneja wake wakawasilisha barua ya kuvunja mkataba Yanga SC.
Ghafla mbele ya waandishi wa habari , Benno akakabidhiwa milioni 2 kutoka kwa Cyprian Msiba kisha akaahidi sasa atarejea kambini kuitumikia Yanga ndipo akaonana na rungu zito la Zahera.
Mpaka hapo utaweza kugundua kwanini Mwinyi Zahera anagoma kumrudisha kikosini japo moyoni mwake anatamani sana kuwa na golikipa kama Benno kikosini mwake ila anatambua hasara ya kumpokea ni kubwa kuliko kumkataa, ukizingatia yeye ndiye aliyebeba maono ya timu! vijana wote ambao hawajalipwa lakini maslahi yao wameweka kando nao wanaufuatilia huu mchezo!
USHAURI WANGU!
Mwinyi Zahera ni muwakilishi wa hisia za kikosi chake, Kamwe Benno asitegemee msamaha binafsi kutoka kwa Zahera! Benno amewakosea na kuwasaliti wachezaji wenzie, Benchi la ufundi, viongozi na mashabiki wa Yanga SC! anachopaswa kufanya ajitokeze yeye binafsi na kulisimamia hili swala liishe aache kusemewa, aambatane na ndugu yake wa karibu wakawaombe msamaha wachezaji huko ndipo msamaha wake utaweza kupatikana sio kwa Zahera, wachezaji wakimsamehe kwa dhati wao ndio wataongea na mwalimu! kwa jinsi Zahera anavoishi na wanaye msitegemee akawa mwamuzi katika hili.
Hili jambo sio dogo kama mdhaniavyo, likichukuliwa kirahisi laweza kuleta mpasuko katika kikosi chetu na kuharibu heshima aliyojijengea mwalimu wetu, Benno acha kujiona star na kuamini nguvu ya mashabiki ndio itakayokurejesha kikosini! Omba msamaha wewe binafsi , kwa dhati kabisa watafute wachezaji, benchi la ufundi waombe msamaha amini nakwambia hao ndio wana password za kureset msimamo wa Zahera.
- Hissan Salum Iddi