Yanga SC kuingia kambini leo kujiwinda dhidi ya Biashara United

Yanga SC kuingia kambini leo kujiwinda dhidi ya Biashara United
Wachezaji wa Yanga SC wale wa kikosi cha kwanza wanaingia kambini leo kujiandaa na mchezo wao wa kombe la FA dhidi ya Biashara United.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema wanamini watafanya vizuri katika mchezo wao kutokana na maandalizi ambayo wameaanza kuyafanya.

"Leo tunaingia kambini rasmi kwani mwanzo timu ilikuwa inafanya mazoezi na wachezaji wanarejea nyumbani ila kwa sasa tunataka wawe sehemu moja ili kujenga timu vizuri," alisema Ten.

Mchezo huyo utachezwa Januari 31 mwaka huu uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga SC wanarudi katika michuano hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kutolewa mapema kwenye michuano ya SportPesa.